• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
NZEGA TOWN COUNCIL
NZEGA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Nzega

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • Origin
      • Ukubwa wa Eneo
      • Watu wa Eneo Husika
      • Hali ya Hewa
      • Shughuli za Kiuchumi
      • Orodha ya Madiwani
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mkakati
  • Utawala
    • Muundo wa Tasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Miji, Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Takwimu, Usimamizi na Ufuatiliji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio Vya Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
  • Huduma Mbalimbali
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha wa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Maadili
      • Ukimwi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kukutana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Miongozo
  • Kituo Cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Wananchi wa Nzega watakiwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kupiga kura.

Tarehe Iliyowekwa: October 11th, 2024


Ikiwa ni siku chache baada ya Makamu wa Rais, Dkt. Philip Isdor Mpango, kuwataka wakazi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura na baadaye kupiga kura, tayari wito huo umeendelezwa na viongozi wengine wa ngazi ya jamii.

“Nawataka bodaboda wenzangu, familia zao na wananchi kwa ujumla kutumia muda uliotolewa kujiandikisha na kupiga kura kwenye daftari maalum kwa muda uliopangwa. Hii ni haki ya kikatiba ya kuchagua viongozi tunaowataka,” alisema Yohana Bujilima, Mwenyekiti wa Kikundi cha Waendesha Bodaboda eneo la Ushirika Mjini Nzega.

Bujilima aliendelea kuwaasa bodaboda wenzake na vijana kwa ujumla kufika kwenye vituo vya kujiandikisha wakiwa watulivu na kufuata utaratibu uliowekwa na wasimamizi wa zoezi hilo bila kusababisha vurugu.

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Humbi, ulioko Kata ya Nzega Mjini Magharibi, Bw. Charles Makala, aliwahamasisha wakazi wa mtaa wake kuwa kujiandikisha na kupiga kura ni jambo muhimu sana na wasikose kutumia vizuri nafasi hiyo ya kushiriki kwenye uchaguzi.

“Tujitokeze kwa wingi maana tunahitaji kuchagua viongozi wa serikali za mtaa wanaotufaa. Tuitumie nafasi hiyo vizuri sana kwa faida yetu wenyewe,” alisema.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Ipilili, Bi Elizabeth Msengi, alisema ofisi ziko wazi kwa siku kumi na moja zilizotengwa kwa ajili ya zoezi hilo. Akiongea na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini mtaani Ipilili, Bi Msengi alisema ofisi ziko wazi, hivyo wananchi wasisite kujitokeza kwa wingi.

Zoezi la kuandikisha wapiga kura litaendeshwa kuanzia tarehe 11 hadi 20 Oktoba mwaka huu, huku zoezi la kupiga kura likitarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba. Katika zoezi hilo, wananchi wa Nzega na Watanzania kwa ujumla watachagua wenyeviti na wajumbe wa vijiji, mitaa, na vitongoji.

Imeandaliwa na James Kamala, Afisa Habari – Nzega Mji.

Matangazo

  • FOMU YA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2021 December 17, 2020
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA October 01, 2019
  • KOROSHO- ZAO LA KIMKAKATI July 23, 2020
  • MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA HALMASHAURI YA MJI NZEGA December 16, 2022
  • Onesha Yote

Habari Mpya

  • WALIMU 184 AJIRA MPYA WAPATA MAFUNZO ELEKEZI

    July 09, 2025
  • KITUO CHA AFYA KITENGWE KIMEKUWA MKOMBOZI KWA WAKAZI WA KATA YA MWANZOLI NA MAENEO YA JIRANI

    July 03, 2025
  • WATUMISHI WA MJI WA NZEGA WAPATA MAFUNZO YA E-UTENDAJI

    June 27, 2025
  • MJI WA NZEGA WAPATA HATI SAFI

    June 19, 2025
  • Onesha Yote

Video

JARIDA KITUO CHA AFYA ZOGOLO & BULUNDE SEKONDARI
Video Nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Matukio
  • Matangazo
  • Zabuni

Kurasa zinazofanana

  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tabora RS
  • TAMISEMI
  • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)

    Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA

    Simu ya Mezani: +255677003373

    Simu ya Mkononi: +255677003373

    Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Binafsi
    • Mlalamikaji
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma

Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017